Katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani tarehe 29/09/2018 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) wafanya upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akimsikiliza mkazi wa Kigamboni aliyejitokeza kupima magonjwa ya moyo pamoja na kupata elimu ya afya bora ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Jumla ya watu 300 walipimwa afya zao ambapo 16 walikutwa na matatizo ya moyo ambayo yalihitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akimsalimia mmoja wa watoto waliojitokeza kupima afya zao wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya