Posts

Showing posts from September, 2018

Katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani tarehe 29/09/2018 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) wafanya upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akimsikiliza mkazi wa Kigamboni aliyejitokeza kupima magonjwa ya  moyo pamoja na kupata elimu ya afya bora ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Jumla ya watu 300 walipimwa afya zao ambapo 16 walikutwa na matatizo ya moyo ambayo yalihitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akimsalimia mmoja wa watoto waliojitokeza kupima afya zao wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya

JKCI Kutambulika Kimataifa kwa Kazi Bora za Upasuaji wa Moyo

Image
Huduma bora za matibabu pamoja na upasuaji wa moyo zimeifanya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)   kutambulika kimataifa na hivyo wataalamu wengi kutoka nje ya nchi kuvutiwa   kwenda kufanya kambi maalum za   matibabu   ya moyo kwa kushirikiana na madaktari wa Taasisi hiyo. Hayo yamesemwa leo   na Mwakilishi wa Mufti,Sheik Hassan Said Chizenga wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya   Misaada (IIRO) ya nchini Saudi   Arabia ambao wako JKCI   katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo. Sheik Chizenga alisema   Taasisi ya Moyo   imekua kimbilio kwa wagonjwa wa   Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kutokana na huduma bora za matibabu ya moyo zinazolewa   kiufanisi. “Taasisi hii imekua kioo si kwa Afrika tu bali Dunia nzima kwa kutoa huduma ya matibabu ya Afya ya moyo na upasuaji kwa wagonjwa ambao ni watanzania na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati” ,alisema Sheik Chizenga. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi M