JKCI Kutambulika Kimataifa kwa Kazi Bora za Upasuaji wa Moyo
Huduma bora za matibabu pamoja na upasuaji wa moyo zimeifanya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutambulika kimataifa na hivyo wataalamu wengi kutoka nje ya nchi kuvutiwa kwenda kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa kushirikiana na madaktari wa Taasisi hiyo. Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa Mufti,Sheik Hassan Said Chizenga wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia ambao wako JKCI katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo. Sheik Chizenga alisema Taasisi ya Moyo imekua kimbilio kwa wagonjwa wa Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kutokana na huduma bora za matibabu ya moyo zinazolewa kiufanisi. “Taasisi hii imekua kioo si kwa Afrika tu bali Dunia nzima kwa kutoa huduma ya matibabu ya Afya ya moyo na upasuaji kwa wagonjwa ambao ni watanzania na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati” ,ali...
Comments
Post a Comment