Posts

Showing posts from October, 2018

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Balsam Care & Care la nchini Saudi Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila kufungua kifua

Image
Daktari wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Balsam Care & Care  la nchini Saudi Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo katika  paja katika kambi maalum ya matibabu inayofanyika kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 26 wamefanyiwa upasuaji huo na hali zao zinaendelea vizuri. Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Balsam Care & Care  la nchini Saudi Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika  kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo.  Jumla ya wagonjwa 10 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na hali zao zinaendela vizuri.

JKCI yawafanyia upasuaji wa Moyo wagonjwa 36 bila kufungua kifua

Jumla ya wagonjwa 36   wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na bila kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi ya Moyo    Jakaya Kikwete (JKCI). Upasuaji huo unafanywa na madaktari bingwa wa moyo wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Albalsam   Care & Care la nchini Saudi Arabia ambapo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua ni 10 na bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo katika    paja 26. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Bashir Nyangasa alisema wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameshatoka katika chumba cha uangalizi maalum na kurudi wodini kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na matibabu.   “Tunafanya upasuaji wa kubadilisha valvu kwa wagonjwa ambao    valvu zao hazifanyi kazi vizuri, kubadilisha   mishipa ya moyo inayosafirisha damu kutoka m