Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul aipongeza Taasisi ya Moyo Nchini
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepongezwa kwa jitihada zake inazozifanya za kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa kutoa huduma bora za matibabu, elimu na ushauri wa jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo. Pongezi hizo zimetolewa jana na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kuangalia huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa kwa wagonjwa. Mhe. Verheul a lisema Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni moja ya Taasisi zinazofanya kazi vizuri ya kutoa huduma ya matibabu ya moyo katika nchi zilizopo Kusini mwa Afrika . Kuhusu Ubalozi wake kushirikiana na Taasisi hiyo katika utoaji wa huduma kwa wananchi alisema ataangalia ni jinsi gani watashirikiana katika programu mbalimbali za afya ambazo zinatolewa hapa nchini kupitia Ubalozi wa Uholanzi. “Wiki tatu zijazo nitaenda nchini Uholanzi ambako tuna mkutano wa mabalozi wote. Kupitia mkutano huo nitaangalia ni Taasisi ipi am